Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuharamisha uhusiano wa kingono wa watu wa jinsia moja ni ukiukwaji wa haki za binadamu:Pillay

Kuharamisha uhusiano wa kingono wa watu wa jinsia moja ni ukiukwaji wa haki za binadamu:Pillay

Takribani nchi 76 zinaendelea na sheria ambazo zinafanya kuwa kosa la jinai kushiriki mapenzi au kuwa na uuhusiano wa kimapenzi wa jinsia moja. Au sheria ambazo zinazuia hali hiyo na hivyo kubagua na kuwachukulia hatua wanawake na wanauume wanaoshiriki ngono za jinsia moja, wanaoshirikia ngono za jinsia zote na watu waliobadilia jinsia. Kamishina mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay amesema sheria hizo sio tuu zinakiuka sheria za kimataifa za haki za binadamu bali pia zinasababisha mateso yasiyo stahili, unyanyapaa, kuchochea ghasia na kuwa kikwazo katika juhudi za vita dhidi ya HIV na ukimwi.

Akizunguma kwenye baraza la haki za binadamu Bi Pillay amezitaka serikali kuwafungulia mashitaka na kuwachukulia hatua watu ambao wanaendeleza ubaguzi na ghasia dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.

(SAUTI YA NAVI PILLAY)