UM watoa wito wa kukomesha ghasia na ubaguzi dhidi ya wapenzi wa jinsia moja

7 Machi 2012
Umoja wa Mataifa umetoa wito wa kukomesha ghasia na ubaguzi wa moja kwa moja dhidi ya mashoga, wanawake wanaofanya mapenzi ya jinsia moja na watu waliobadili jinsia.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema ubaguzi kwa misingi ya mfumo wa kimapenzi na jinsia ni ukiukaji wa sheria za kimataifa.

Akihutubia baraza la haki za binadamu Ban amesema nchi ni lazima zishughulikie ghasia dhidi ya wapenzi wa jinsia moja, zikomeshe hali ya kuwa ni uhalifu kushiriki ngono za watu wa jinsia moja, zipige marufuku ubaguzi unaohusiana na masuala ya ngono za jinsia moja na pia zielemishe jamii.

Katibu Mkuu amesema anapinga majaribio ya baadhi ya nchi wahisani kuhusisha misaada yao ya  kimataifa ya baadaye na suala la haki za wapenzi wa jinsia moja.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter