Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Njia tano za kukabiliana na matatizo ya afya ya jamii yatokanayo na vyakula visivyofaa

Njia tano za kukabiliana na matatizo ya afya ya jamii yatokanayo na vyakula visivyofaa

Mifumo ya chakula duniani inasababisha maradhi ameonya mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na haki ya chakula Olivier De Schutter.

De Schutter amesema kila mtu mmoja kati ya saba duniani ana utapia mlo, lakini wengi zaidi wanakabiliwa na matatizo ya njaa ya kukosa vyakula bora, huku watu bilioni 1.3 wanasumbuliwa na matatizo ya kuwa na uzito wa kupindukia.

Amesema matatizo haya yatokanayo na lishe au vyakula visivyofaa yanapaswa kuwa na mfumo maalumu wa kuyashughulikia, hasa kuhakikisha lishe duuni na vyakulaa visivyofaa yanapata ufumbuzi.

Afisa huyo ameyasema hayo wakati akiwasilisha ripoti yake katika baraza la haki za binadamu mjini Geneva.

Amesema pamoja na kupata suluhu ya muda mrefu wataalamu wanaendelea kutumia njia mbadala kuhakikisha watu wanapata lishe inayostahili ikiwa ni pamoja na tembe, mikakati ya mapema ya kurutubisha afya kwa wanaokosa madini yanayohitajika mwilini, kuwapa vidonge vya kupunguza nene walio na uzito wa kupindukia, kutoa ushauri wa kubadili mfumo wa maisha na kuendelea kuzingatia ni kiasi gani cha chakula kinaliwa na watu wenye uzito kupita kiasi.

Katika ripoti yake ametaja mambo matano ya kuyazingatia katika lishe kwa mafia yaliyoendelea na yanayoendelea, kwanza ni kutoza ushuru bidhaa zisizofaa kwa afya, kufuatilia vyakula vyenye mafuta , sukari na chumvi nyingi, kupinga matangazo ya vyakula visivyofaa, kuzingatia ruzuku za kilimo na kuunga mkono bidhaa zinazozalishwa mashinani.