Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM washangazwa na picha za mateso kutoka nchini Syria

UM washangazwa na picha za mateso kutoka nchini Syria

 

Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa inasema kuwa imeshangazwa na picha za video kutoka nchini Syria zinazoonyesha wagonjwa walioteswa wanapoendelea kupata matibabu kwenye hospitali moja ya kijeshi.

 Ofisi hiyo inasema kwamba ripoti kama hizo za kuteswa kwa wafungwa pia zimetoka kwa tume ya uchunguzi ya uchunguzi iliyoteuliwa kuchunguza hali nchini Syria.

Tume hiyo ilisema kuwa wanajeshi waliovalia kama madaktari walihusika kutekeleza mateso hayo.

 Kwa sasa raia wamegeukia vituo vidogo vya afya ili kupata matibabu na ambavyo hata hivyo havina uwezo wa kutibu watu waliojeruhiwa.

 Rupert Colville ni kutoka ofisi ya haki za binadamu.