Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Viongozi wa dunia kujadili mawasiliano ya teknolojia mjini Doha

Viongozi wa dunia kujadili mawasiliano ya teknolojia mjini Doha

Wajumbe wakiwemo zaidi ya wawakilishi ishirini wanaowajumuisha marais na wakuu wa serikali, mawaziri 27 na wakuu wa makampuni makubwa zaidi kwenye masuala ya teknolojia ya mawasiliano duniani wanakutana juma hili mjini Doha kujadili mikakati na sera ambazo zitahakikisha kuwepo masoko na maendeleo kwenye eneo lote la nchi za kiarabu.

Mkutano huo unaoandaliwa na taifa la Qatar pia utakuwa sehemu muhimu ya kutangazia ahadi mpya kutoka kwa serikali na wasomi za kuboresha teknolojia ya mawasiliano.

Mkutano huo utahudhuriwa na mawaziri 27 na mawaziri manaibu kutoka nchi zikiwemo Algeria, Azerbaijan, Bahrain, Comoros, Djibouti, Misri, Iraq, Jordan, Kuwait, Lebanon, Libya, Mauritania, Morocco, Oman, Saudi Arabia, Somalia, Sudan, Tunisia, Miilki ya nchi za kiarabu, Yemen na utawala wa Palestina.