Michelle Bachelet kwenda Morocco kuadhimisha siku ya wanawake duniani

6 Machi 2012
Mkuu wa kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachoshughulikia masuala ya wanawake Michelle Bachelet anatazamiwa kuelekea nchini Morocco ambako anaungana na wananwake wa eneo hilo kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.

Akiwa nchini humo anatazamia kuweka zingatio kubwa juu ya wanawake kushiriki kwenye majukwaa ya maamuzi.

Anatazamia kuongeza msukumo kuhusu nafasi ya wanawake kwenye majukwaa ya kisiasa na wakati huo huo akitoa wito wa wanawake kupewa fursa sawa kwenye mabaraza ya maamuzi.

Ama anatazamia kuhimiza mamlaka za kidola kufungua milango kwa makundi ya wanawake ili waweze kushiriki kikamilifu kwenye michakato ya kidemokrasia.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud