Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Somalia bado iko hatarini: Ban Ki-moon

Somalia bado iko hatarini: Ban Ki-moon

Ingawa hali ya kibimadamu imeboreshwa nchini Somalia, nchi hii ya Pembe ya Afrika bado iko hatarini.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameyasema haya  katika mjadala  wa Baraza la Usalama juu ya Somalia ambao umefanyika leo jumatatu.

Bw. Ban amesema kumekuwa na maendeleo katika mchakato wa amani, akitoa mfano wa mikutano miwili iliyofanyika kuhusu Somalia mwezi Februari.

Amesema mkutano wa kujadili katiba ya Somalia uliofanyika mjini Garowe, Puntland na ule wa London wa kuongeza msaada kwa nchi hii ulitoa matumaini ya kuleta utulivu nchini.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

Katibu Mkuu amesisitiza umuhimu wa kuisaidia serikali ya mpito ya Somalia kupanua mamlaka yake kuelekea kusini na katikati mwa Somalia ili kuwaangamiza wanamgambo wa Al-Shabaab.