Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ujumbe wa UNEP wakamilisha tathmini ya tetemeko lililotokea Japan

Ujumbe wa UNEP wakamilisha tathmini ya tetemeko lililotokea Japan

Shirika la Umoja wa Mataifa la mazingira UNEP limehitimisha ziara ya ujumbe wa wataalamu wa kimataifa katika maeneo yaliyoathirika na tetemeko la ardhi na tsunami nchini Japan mwaka 2011.

Ziara hiyo ilijikita katika kuangalia jinsi taka zinavyodhibitiwa baada ya tetemeko.

Ikiwa katika mkesha wa maadhimisho ya mwaka mmoja wa tetemeko hilo UNEP inasema kumepigwa hatua kubwa katika kukusanya na kuhifadhi mamilioni ya tani ya taka zilizosababishwa na tetemeko na tsunami na kwamba Japan imeweka viwango vipya vya kudhibiti taka. Tetemeko na tsunami Japan ilikatili maisha ya watu zaidi ya 15,000, kuharibu miji na vijiji na kusababisha taka tani milioni 29. Watu 3305 bado hawajapatikana hadi sasa.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)