Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Congo Brazaville yaomba msaada wadharura wa kimataifa

Congo Brazaville yaomba msaada wadharura wa kimataifa

Maaafisa wa serikali ya Jamhuri ya Congo wameomba msaada wa jumuiya ya kimataifa baada ya kutokea ajali ya mlipuko katika bohari la silaha na kukatili maisha ya watu takribani 150 na kujeruhi wengine 1500.

Mlipuko huo ulitokea katika mji mkuu Brazzaville na makundi ya waokozi bado yanaendelea kuwatafuta manusura.

Mlipuko huo pia umeathiri makazi na majengo, na hospitali zinakabiliwa na wakati mgumu katika kukidhi mahitaji ya idadi kubwa ya majeruhi.

Hadi sasa maiti 146 zimehifadhiwa katika chumba cha maiti na idadi inatarajiwa kuongezeka Arsene Severin ni mwandishi wa habari wa Radio ya Umoja wa Mataifa ya Okapi mjini Brazzaville.

(SAUTI YA ARSENE SEVERIN)

Kwa mujibu wa serikali bohari hilo linahifadhi silaha za vita yakiwemo makombora. Serikali imelaumu hitilafu ya nyaya za umeme kuwa ndio chanzo cha mlipuko huo.

Muungano wa Afrika umetuma salamu za rambirambi na kuitaka jumuiya ya kimataifa kulisaidia taifa hilo.