Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maisha ya mtoto kutoka sehemu maskini mjini Nairobi kuangaziwa

Maisha ya mtoto kutoka sehemu maskini mjini Nairobi kuangaziwa

Msichana moja wa umri wa miaka 13 pamoja na wenzake wanatarajiwa kuungana na shirika la mpango wa chakula duniani WFP kwenye mawasiliano kwa njia ya video ya moja kwa moja ambapo watazungumzia maisha yao kwenye vitongoji maskini vya mji mkuu wa Kenya, Nairobi.

Molly ameelezea kuhusu maisha yake ya kila siku kwenye mtaa maskini wa Mathare kwenye kanda zenye vichwa “Ulimwengu wa Molly” ambapo atawasimulia watoto kutoka shule moja ya kimataifa mjini Rome kuhusu maisha yake.

Molly amepokea chakula kutoka WFP akiwa shuleni tangu miaka minne iliyopita. Mkurugenzi wa mawasilianio na ushirikiano kwenye shirika la UNESCO Nancy Roman anasema kuwa kumlisha mtoto msichana chakula akiwa shuleni ni kufanikisha ndoto zake siku za baadaye.