Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya matatizo ya kiuchumi uandikishaji hati miliki umevunja rekodi 2011: WIPO

Licha ya matatizo ya kiuchumi uandikishaji hati miliki umevunja rekodi 2011: WIPO

Licha ya mazingira magumu ya kiuchumi uandikishaji wa kimataifa wa hati miliki umevunja rekodi mwaka 2011, ambapo kumekuwa na maombi 182,000 limesema shirika la kimataifa linalohusika na masuala ya hati milikI WIPO.

Ongezeko hilo la maombi linawasilisha ukuaji wa asilimia 10 ikilinganishwa na maombi yaliyowasilishwa mwaka 2010.

Mkurugenzi mkuu wa WIPO Francis Gurry anasema ongezeko la idadi ya masuala ya hati miliki ni ishara kwamba makampuni yanatambua umuhimu wa ubunifu katika mikakati yao ya maendeleo.

Ameongeza kuwa chumi wa Asia taratibu unakuwa kitovu cha ubunifu, ukizisukuma kando Marekani na Ulaya.

(SAUTI YA FRANCIS GURRY)

Marekani, Japan, Ujerumani, Uchina na Korea ndizo zilizo na idadi kubwa ya maombi ya hati miliki na China ndio iliyokuwa na idadi kubwa zaidi mwaka 2011 huku kampuni ya Panasonic ya Japan ikiandikisha idadi kubwa ya maombi yaliyofanywa na makampuni.