Wakulima wa vijijini watakiwa kuwa na ushirikino wa kuzalisha chakula

2 Machi 2012

Serikali kwenye nchi zinazoendelea ambazo zinakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula zimetakiwa kufanya ushirikiano na wazalisha na pia kuwa na ushirikiano ili kupambana na njaa.

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya usalama wa chakula na lishe David Nabarro anasema kuwa mashirika kama hayo yatawawezesha wazalishaji wadogo kuchangia kabisa katika upatikanaji wa chakula kwa wao wenyewe na hata kimataifa.

Nabarro ameongeza kuwa uwekezaji kwa wakulima wadogo unahitajika kuboresha usalama wa chakula na kuongeza mapato kwenye sehemu za vijijini.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter