Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya watu wanaoishi chini ya dola moja kwa siku yapungua

Idadi ya watu wanaoishi chini ya dola moja kwa siku yapungua

 

Benki ya dunia inasema kuwa idadi ya watu wanaoishi kwa chini ya dola 1.25 kwa siku kwenye nchi zinazoendelea inaripotiwa kupungua kati ya mwaka 2005-2008. 

Takwimu hizo ambazo utafiti wake ulichukua muda wa miaka mitatu ndio wa kwanza tangu benki ya dunia ianzishe utafiti kuhusu umaskini. 

Takriban watu bilioni 1.29 waliishi chini ya dola moja 1.25 kwa siku mwaka 2008 ikiwa ni asilimia 22 ya watu wanaoishi kwenye nchi zinazoendelea. Utafiti huo uliendeshwa kwenye nyumba 850 kwenye nchi 130.