Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

China na UNESCO zatia sahihi makubaliano ya kuboresha elimu Afrika

China na UNESCO zatia sahihi makubaliano ya kuboresha elimu Afrika

 

Mkurugenzi wa shirika la elimu, Sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa UNESCO Irina Bokova pamoja na naibu waziri wa ulimu na mwenyekiti wa tume ya kiataifa ya UNESCO nchini China Hao Ping wametia sahihi makubaliano ya kuchangisha dola milioni 8 za kufadhili elimu na maendeleo barani Afrika kwa muda wa zaidi ya miaka minne.

Ufadhili huo ambao ndio wa kwanza kabisa kufanywa na China ulijadiliwa kwanza wakati Bokova alipokutana na rais wa china Hu Jintao mwezi Agosti mwaka uliopita.

Bokova amesema kuwa hilo ni jambo la kihistoria linalolipa matumaini shirika hilo akiongeza kuwa ufadhili huo utaboresha elimu ambayo ni ajenda yao kuu.