Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yazindua mwongozo wa kupunguza vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu

WHO yazindua mwongozo wa kupunguza vifo vinavyosababishwa na ugonjwa wa Kifua Kikuu

Takriban maisha ya watu 910,000 yameokolewa kwa muda wa zaidi ya miaka sita iliyopita kutokana na kuboreka kwa huduma za matibabu dhidi ya maradhi ya kifua kikuu na ukimwi ambazo huwazuia watu wanaoishi na virusi vya ukimwi kutokana na ugonjwa wa kifua kikuu.

Hii ni kulingana na takwimu za afya za dunia nzima zilizotolewa hii leo. Pia shirika la afya duniani WHO hii hiileo linatoa mpango wa kuzuia , kupima na matibabu ya ugonjwa wa kifua kikuu na HIV. Ugonjwa wa kifua kikuu husababisha vifo vingi zaidi miongoni mwa watu wanaoishi na virusi vya ukimwi.