Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Raia zaidi wa Mali wakimbilia Mauritania na Burkina Faso

Raia zaidi wa Mali wakimbilia Mauritania na Burkina Faso

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR linasema kuwa mataifa ya Mauritania na Burkina Faso yamekuwa yakishuhudia idadi kubwa ya wakimbizi kutoka Mali wanaokimbia mapigano kati ya waasi wa Tuareg na wanajeshi wa Mali.

Karibu watu 31,000 wameikimbia Mali na kuingia nchini Mauritania huku wengine 20 wakiandikishwa nchini Burkina Faso. Mataifa hayo mawili yanaripotiwa kupokea wakimbizi 2000 kutoka mali kila siku. Andrej Mahecic kutoka UNHCR wamekimbia makwao kutokana na hofu kwamba huenda wakakutwa kwenye mapigano.

(SAUTI YA ANDREJ MAHICIC)