Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yawasaidia watu 1400 kurudi Sudan Kusini

IOM yawasaidia watu 1400 kurudi Sudan Kusini

Gari moshi moja kupitia usaidizi kutoka kwa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na ambalo limewabeba watu 1400 raia wa Sudan Kusini wanaorejea nyumbani kutoka mji wa Khartoum liko njiani kwa safari ambayo itachukua muda wa siku kumi ikielekea maeneo ya Aweil na Wau nchini Sudan Kusini.

Hili ndilo gari moshi la kwanza kabisa kuondoka mjini Khartoum kuelekea kusini tangu kusainiwa kwa makubaliano kati ya Sudan na Sudan Kusini mapema mwezi Februari yaliotaka kuwepo amani wakati wa kurejea nyumbani kwa watu hao.

Wengi wa abiria hao 1400 wanaosafiri wamekuwa wakiishi nje kwa zaidi ya mwaka mmoja wakisubiri msaada wa serikali wa kuwasafirisha kwenda Sudan Kusini Jumbe Omar Jumbe ni afisa wa IOM.