Shirika la wanawake wa UM kutoa dola milioni 10.5 kwa miradi ya kuwainua wanawake

2 Machi 2012

Shirika la wanawake wa Umoja wa Mataifa wanatarajiwa kutoa dola jumla ya dola milioni 10.5 kwa minajili ya kuinua masuala ya wanawake ya kiuchumi na kisiasa kwa wanawake wa bara la Afrika, Asia na Pacific , America Kusini Caribbean, Ulaya na Asia ya kati.

Shirika hilo linasema kuwa fedha zitaanzisha miradi ambayo itayaboresha maisha ya wanawake na watoto wasichana na kuwawezesha wanawake kuwania nyadhifa za kisiasa ili kuweza kuinua familia zao.

Mkurugenzi wa shirika hilo Michelle Bachelet anasema kuwa miradi hiyo ni muhimu kwa wanawake na pia inasaidia kulinda usawa wa kijinsia, demokrasia na masuala ya uchumi.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud