Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR yalaani mauji ya mkimbizi aliyekua katika juhudi za kuomba hifadhi, Indonesia

UNHCR yalaani mauji ya mkimbizi aliyekua katika juhudi za kuomba hifadhi, Indonesia

Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa limelaani na kuelezea masikitiko yake kutokana na kuuliwa kwa raia mmoja wa Afghanistan ambaye alikuwa katika juhudi za kuomba hifadhi ya kisiasa huko Indonesia.

Duru za habari zinasema kuwa, mamlaka ya Indonesia iliwatia kuzuizini raia sita wa Afghanistan ambao waliingia nchini humo katika jitihada zao za kusaka hifadhi zaidi.

Ripoti ya kupoteza maisha kwa raia huyo zimepokelewa kwa masikitiko makubwa na shirika hilo la Umoja wa Mataifa ambalo limesema kuwa mamlaka ya Indonesia yaliziendea kinyume sheria za kimataifa.

Kuna taarifa kwamba raia wengine watatu wamelazwa hospitali kutokana na kukabiliwa na majeraha makali. Wengine wanaendelea kushikiliwa kizuizini.