Skip to main content

Maelfu washiriki katika mbio za marathan za Gaza:UM

Maelfu washiriki katika mbio za marathan za Gaza:UM

Mamia kwa maelfu wamejitokeza huko Gaza kushiriki mbio za marathon ambazo zimeandaliwa maalumu kwa ajili ya kuchangisha fedha kuwakirimu makundi ya watoto.

Watoto zaidi 2000, na kundi la watu wazima wapato 500 walijikoza kwenye mbio hizo na kuzunguka katika maeneo kadhaa ya ukanda wa Gaza.

Mbio hizo zilizoandaliwa na shirika la kuhudumia wakimbizi wa Palestina UNRWA ni maalumu kwa kukusanya fedha zitakazotumika kugharimia maandalizi ya michezo ya watoto katika kipindi cha majira ya joto.

Wengi walioshiriki mbio hizo ambao baadhi wakilimbia umbali wa kilometa 3, wameelezea furaha yao na kusema kuwa imekuwa fursa nzuri ya kuleta mshikamano na umoja.