Wanawake bado wanaendelea kutupa au kutelekeza watoto Afrika

2 Machi 2012

Kila kunapokucha hasa kwenye nchi za bara Afrika kunaripotiwa visa vya kutupwa kwa watoto wachanga mara wazaliwapo.

Na ukatili huo hufanywa mara nyingi na wazazi ambao ama hawana mipango ya kuchukua majukumu ya kuwalea watoto hao au kutokana na sababu moja au nyingine, huku wengi wakiokotwa barabarani , kwenye majaa ya taka na wengine wakiwa wametelekezwa kwenye mahospitali.

Hali hii imesababisha kuibuka kwa mashirika mengi yanayojitolewa kuwachukua watoto hawa na kuwalea hadi kufikia umri wa utu uzima. Shirika la Baby Blessing Children's home lililo na makao yake mjini Nairobi nchini Kenya ni kati ya mashirika yaliyochukua majukumu ya kulea watoto hao waliotupwa au kutelekezwa na wazazi wao tangu wakiwa wachanga hadi wanapohitimu miaka 18.

Pia linawasaidia watoto wanaorandaranda mitaani na kuwawezesha kupata mkate wao wa kila siku. Mbali ya hayo linawasidia wanawake wanaoishi na virusi vya ukimwi ambao hawana uwezo wa kujitafutia chakula wala kuweza kugharamia madawa wanayotumia ya kupunguza makali ya ukimwi..

Mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi alitembelea shirika la Babby Blesing ili kufahamu zaidi kuhusu jukumu, mchango na msaada wao kwa jamii.

(MAKALA NA JASON NYAKUNDI)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter