Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maambukizi ya kipindupindu yameongezeka kwa mara kumi zaidi ya takwimu za hapo awali

Maambukizi ya kipindupindu yameongezeka kwa mara kumi zaidi ya takwimu za hapo awali

Shirika la Afya Duniani WHO limesikitishwa na takwimu za ripoti ya maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu ambazo zimeongezekakwa mara kumi zaidi ikilingananishwa na ripoti ya hapo awali.

Kulingana na matokea yaliyochapishwa kwenye makala ya kila mwezi ya WHO, jukwaa la wataalam wa hali ya afya ya umma wamewasilisha utafiti kwamba takriban watu milioni 3 wanaambukizwa ugonjwa wa kipindupindu kila mwaka huku watu 100,000 wakifariki.

WHO inasema kwamba nchi zinapaswa kuripoti mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu hii ni kuambatana na sheria za kimataifa za afya, lakini shirika hilo hupokea asilimia kumi tu ya ripoti ya maambukizi.

Tarik Jasarevic, msemaji wa WHO amesema kwamba nchi nyingi hazina teknologia za utafiti na maabara ya kuugundua ugonjwa wa kipindupindu na kwa hivyo huripotiwa kama ugonjwa wa kuendesha.