Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM umewataka wachomaji wa Quaran nchini Afghanistan kuwajibika

UM umewataka wachomaji wa Quaran nchini Afghanistan kuwajibika

Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu nchini Afghanistan amesema waliohusika na kuchoma Quaran wanafaa kuwajibika.

Jan Kubis amesema haya katika mkutano mjini Kabul kufuatia uchunguzi wa ndani. Wakati huo huo pia amewashtumu wale ambao wametumia kitendo hiki kama kisingizio cha kuanzisha maandamano ya vurugu.

Bw. Kubis amesema ingawa serikali ya Marekani imeomba msamaha lakini bado juhuzi zaidi zinahitajika.

(SAUTI YA  JAN KUBIS)

Baada ya kuomba msamaha na baada ya uchunguzi, lazima hatua ya nidhamu ichukuliwe. Wale waliofanya kosa hili wanapaswa kuwajibika. Kwa hivyo natumai kuwa baada ya matokeo ya uchunguzi kutolewa hatua ya nidhamu itachukuliwa.

Wiki hii, mpango wa Umoja wa Mataifa wa Afghanistan UNAMA, umewaondoa wafanyakazi wake kwa muda kutoka eneo la Kunduz kwa sababu ya vurugu.