Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni ya Kimataifa dhidi ya mabomu ya kutegwa ardhini yazinduliwa

Kampeni ya Kimataifa dhidi ya mabomu ya kutegwa ardhini yazinduliwa

Katika maadhimisho ya 13 ya mkataba wa kimataifa kupinga mabomu ya kutegwa ardhini kuwa sheria, dunia imeungana pamoja tena kuzitaka serikali kukomesha kabisa mabomu hayo ambayo yanasababisha athari kubwa katika maisha ya watu kwa kupitia kampeni iliyozinduliwa iitwayo “Lend Your Leg” au azimisha mguu wako.

Mwaka 2010 takwimu zinaonyesha kwamba kwa wastani watu 12 walikuwa wanauawa kwa siku au kujeruhiwa na mabomu ya kutegwa ardhini katika sehemu mbalimbali duniani.

Uzinduzi wa kampeni hii unaanza wiki tano za kuchukua hatua katika nchi mbalimbali kwa ushirikiano wa Umoja wa Mataifa, kampeni ya kimataifa kupinga mabomu ya ardhini ICBL na shirikisho la chama cha msalaba mwekundu na mwezi mwekundu hadi tarehe 4 Aprili siku ambayo ni siku ya Umoja wa Mataifa inayoadhimishwa kila mwaka kuelimisha kuhusu mabomu ya ardhini na kuchukua hatua.

Mkurgenzi wa ICBL Kasia Derlicka anasema mabomu ya kutegwa ardhini bado ni tishio kubwa katika maisha ya maelfu ya watu ulimwenguni.

(SAUTI YA KASIA DERLICKA)