Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taasisi na mashirika imara vijijini vitasaidia kupambana na njaa na umaskini: FAO/IFAD

Taasisi na mashirika imara vijijini vitasaidia kupambana na njaa na umaskini: FAO/IFAD

Mashirika imara vijijini kama makundi ya wazalishaji na vyama vya ushirika ni muhimu sana kwa kupunguza njaa na umasikini.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la chakula na kilimo FAO na mfuko wa kimataifa kwa ajili ya maendeleo ya kilimo IFAD ushirika huo unawaruhusu wakulima wadogowadogo kubeba jukumu muhimu la kwenda sambamba na ongezeko la mahitaji ya chakula katika ngazi ya jamii, kitaifa na kwenye masoko ya kimataifa huku wakiimarisha uchumi wao, na fursa za kijamii, kisiasa na kiuchumi.

Mtazamo huu umetokana na matokeo ya ufatifi uliofanywa na kuchapishwa na FAO na IFAD katika nchi kadhaa. George Njogopa anaripoti.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)