Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM wawateua maafisa wawili kukamilisha kesi za uhalifu wa kivita

UM wawateua maafisa wawili kukamilisha kesi za uhalifu wa kivita

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limemteua mwendesha mashataka kwenye mpango wa mwaka 2010 ambaye atakamilisha kesi za mahakama ya Umoja wa Mataifa ya iliyokuwa Yugoslavia ya zamani na Rwanda. Baraza hilo lilifikia uamuzi wa kumteua Hassan Bubacar Jallow raia wa Gambia ambaye ni mwendesha mashataka wa mahakama kuhusu Rwanda ICTR kuwa mwendesha mashstaka wake kwa kipindi cha miaka minne.

Hassan pia ataendelea kuhudumu kama mwendesha mashtaka wa mahakama ya ICTR. Pia Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon alimteua Theodor Meron kutoka Marekani kuwa rais wake kwa kipindi cha miaka minne.