Askari wa UNAMID auawa kwa risasi Darfur

1 Machi 2012

Askari mmoja anayelinda amani katika jimbo lenye mzozo la Darfur, Sudan ambaye ni miongoni mwa askari wa muungano wa vikosi vya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika ameuwawa kwa kupigwa risasa.

Askari wengine watatu wamejeruhiwa wakati mtu asiyejulikana aliposhambulia msafara wa askari hao waliokuwa wakiendesha doria katika eneo la Shearia, lililoko kusini mwa jimbo la Darfur.

Kulingana na msemaji wa muungano wa vikosi hivyo UNAMID, mauwaji ya askari huyo yanafanya jumla ya askari waliopoteza maisha kufikia 36 .

Vikosi hivyo vya kimataifa ambavyo vipo kwenye eneo hilo lenye mzozo tangu 2008 kama jitihada za jumuiya ya kimataifa kuleta hali ya utengamano bado vinakabiliwa na wakati mgumu ambao unakwamisha juhudi za umalizaji mapigano na machafuko.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter