Eneo la Pembe ya Afrika kupata mvua chini ya wastani-UM

1 Machi 2012

Eneo la Pembe ya Afrika linatazamia kupata mvua ya wastani ikiwa na upungufu kwa kuzingatia kiwango cha wastani kilichozoeleka kwenye eneo hilo katika miaka ya hivi karibuni.

Mvua hizo zitazoanza kunyesha kuanzia kipindi cha mwezi March hadi May, hata hivyo hazitaleta nafuu kubwa kwa wananchi wa eneo hilo ambalo hivi karibuni shughuli zao za kilimo zilivurugika vibaya kutokana na hali ya ukame uliojitokeza.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na kitengo cha hali ya hewa cha Umoja wa Mataifa mvua hizo zitasambaa kuanzia Somalia,Djibout, pamoja na maeneo ya mashariki na kaskazini mwa Kenya na maeneo kadhaa ya Ethiopia ikiwemo Kusin na Kaskazini.

Wataalamu wa hali ya hewa kutoka kwenye kitengo hicho wanasema kuwa, maeneo hayo yanatazamia kushuhudia vipindi virefu vya ukame jambo ambalo litaathiri shughuli mbalimbali za kilimo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter