Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la Usalama huenda likawa tena na azimio kuhusu Syria

Baraza la Usalama huenda likawa tena na azimio kuhusu Syria

Baraza la Usalama huenda likawa na azimio tena kuhusu Syria kwa mujibu wa balozi wa Uingereza kwenye Umoja wa Mataifa, ambaye anachukuwa jukumu la Rais wa Baraza la Usalama kwa mwezi huu wa Machi.

Balozi Mark Lyall Grant amesema Baraza la Usalama litakuwa na matukio matatu rasmi kwa mwezi huu. Moja itakuwa ni mkutano wa ngazi ya mawaziri kujadili mabadiliko Mashariki ya Kati na maafisa kadhaa wa nchi za Kiarabu wamealikwa. Pili kutakuwa na kikao maalumu kitakachojikita katika suala la Somalia na mwisho itakuwa ni kikao kuhusu kuendelea kwa mgogoro nchini Sudan. Bwana Lyall Grant pia amesema anatarajia baraza kujadili Syria zaidi ya mara moja katika mwezi huu.

(SAUTI YA LYALL GRANT)

Ameongeza kuwa baraza pia litajadili hali ya Libya na Haiti na kuwa na mjadala maalumu wa kulifanya baraza kujikita zaidi katika kuzuia migogoro zaidi kuliko kukabili machafuko.