Baraza la Haki za Binadamu lataka ghasia zikomeshwe Syria

1 Machi 2012

Baraza la Haki za Binadamu limelaani ghasia na ukiukwaji wa haki za binadamu unaoendelea nchini Syria na kutaka kukomeshwa mara moja kwa kitendo cha majeshi ya serikali kuwaandama waandamanaji wanaoipinga serikali. 

Katika azimio lililopitishwa na wajumbe 37 nchi wanachama, baraza limelaani kile linachosema ni vitendo vya kikatili vya serikali ya Syria ambavyo vimewalazimisha maelfu ya watu kuzikimbia nyumba zao na kusababisha janga la kibinadamu. 

Baraza linataka Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya misaada yapewe fursa ya kufika kwenye maeneo yaliyoathirika ili kufikisha mahitaji yanayohitajkika kwa haraka ya chakula na msaada wa madawa. 

Urusi, Cuba na Uchina wamepinga azimio hilo wakisema linaegemea upande mmoja na halijatoa pendekezo lolote la jinsi gani ya kumaliza ghasia nchini humo. Vladmir Zheglov ni balozi wa Urusi. 

(SAUTI YA VLADMIR ZHEGLOV)

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud