Amos asikitika kwa kutozuru Syria

29 Februari 2012

Mratibu wa huduma za dharura za misaada kwenye Umoja wa Mataifa Valerie Amos ameelezea sikitiko lake kutokana na sababu kwamba hajaitembelea Syria mwenyewe ili kujionea hali ya kibinadamu na kufanya mikutano na maafisa wa ngazi za juu wa nchi hiyo.

Maelfu ya raia wameuawa kwenye oparesheni za serikali dhidi ya wanaoipinga serikali zilizoanza machi mwaka uliopita na kuchacha siku za hivi majuzi.

Amos anasema kuwa aliunga mkono wito wa kamati ya kimataifa ya msalaba mwekundu ICRC wa kutaka kusitishwa ghasia kila siku ili kuweza kutoa nafasi kwa makundi ya kutoa misaada kuweza kuwasaidia majeruhi.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter