Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Changamoto zaingoja serikali mpya nchini Libya

Changamoto zaingoja serikali mpya nchini Libya

Mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya Ian Martin anasema kuwa hata baada ya kuwepo ghasia nchini humo suala lililo wazi ni kwamba watu wa Libya wana nia ya kusonga mbele kupata demkokrasia.  

Akihutubia baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kwa njia ya video kutoka nchini Libya, Martin anasema kuwa kile Libya inachotarajia ni usaidizi wa Umoja wa Mataifa hasa kwenye uchaguzi mkuu unaokuja.

Kwenye siku za hivi karibuni kumekuwa na ghasia mbaya kati ya jamii ya Tabou na Zwaya kwenye mji ulio kusini mwa Kufra ambapo watu 100 wameripotiwa kuuawa na wengine wengi kujeruhiwa.