Ban awataka watu wa Timor-Leste Kufanya uchaguzi kwa amani

29 Februari 2012

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amewataka watu wa Timor-Leste kufanya uchaguzi kwa amani na utulivu. Ban amesema uchaguzi ujao wa Rais ni hatua muhimu kwa taifa hilo katika kudumisha demokrasia.

 Amesema kufanyika kwa uchaguzi huo ni ishara ya hatua iliyopigwa katika muongo mmoja tangu kurejeshwa kwa uhuru ambapo amani na ukuaji wa uchumi vimechukua nafasi ya machafuko na dhiki. Amewataka wasilichukulie kirahisi suala la amani, utulivu na demokrasia.

(SAUTI YA BAN KI-MOON)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter