Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tovuti ni chombo muhimu kwa watu kupata taarifa:Pillay

Tovuti ni chombo muhimu kwa watu kupata taarifa:Pillay

Tovuti imekuwa ni nyenzo muhimu kwa watu kupata taarifa zaidi ya zile zinazotayarishwa na kusambazwa na vyombo vya asili vya habari. Hayo yamesemwa na kamishina mkuu wa haki za binadamu Navi Pillay katika mjadala wa haki ya uhru wa kujieleza katika tovuti uliofanyika Jumatano mjini Geneva.

Amesema wakati huohuo tovuti imesuruhusu watumiaji wote kutoa taarifa, matokeo yake tovuti imebadili vuguvugu la kupigania haki za binadamu, na mataifa hayana tena nguvu za kudhibiti taarifa. Lakini ameonya kwamba lazima uangalifu uwepo.

(SAUTI YA NAVI PILLAY)