Mshauri wa UM wa michezo aunga mkono mpango wa kuruhusu hijab salama katika soko

29 Februari 2012

Katika hatua ya karibuni ya maendeleo katika mchezo wa kandanda kuhusu suala la wachezaji wanawake kuvaa hijab wakati wakiwa kiwanjani , mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu michezo kwa ajili ya maendeleo ya amani Wilfried Lemke amesema anaunga mkono hatua iliyopendekezwa na makamu wa raia wa shirikisho la soka duniani FIFA Mwana mfalme Ali Bin Al Hussein kwa niaba ya shirikisho la kandanda Asia AFC.

Prince Ali Bin Al Hussein anataka sheria za mchezo wa kandanda zifanyiwe tathimini ili kuruhusu hijab salama kwa wachezaji wanawake.

Bodi ya kimataifa ya mpira wa kandanda IFAB ambayo inatunga sheria za kandanda itafanya mkutano wake 126 wa kila mwaka Jumamosi ijayo Machi 3, ambapo katika ajenda za mwaka huu kuna mapendekezo manane ya kufanyia marekebisho sheria za kandanda ikiwemo mjadala kuhusu Hijab.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter