Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bei ya chai kuendelea kupanda kutokana na ongezeko la mahitaji:FAO

Bei ya chai kuendelea kupanda kutokana na ongezeko la mahitaji:FAO

Utabiri wa awali wa mwaka 2012 unaonyesha kuendelea kupanda kwa bei ya chai kwa wasitani wa asilimia 2.2 kwa kilo hapo mwaka 2011 limesema kundi la la shirika la chakula na kilimo FAO la mataifa wazalishaji wa chai.

FAO inasema bei za juu za chai zinaashiria ukweli kwamba mahitaji ya chai ambayo inachukua nafasi kubwa ya uzalishaji duniani yameongezeka na kupita uzalishaji tangu mwaka 2009. Tathimini hiyo imetolewa na kundi la wazalishaji wa chai katika mkutano wa kila mwaka unaofanyika mjini Colombo Sri Lanka. George Njogopa na taarifa kamili.

(RIPOTI YA GEORGE NJOGOPA)