IOM yabaini watoto waliotelekezwa kwenye mpaka wa Chad na Nigeria

29 Februari 2012

Tathimini ya pamoja iliyofanywa na shirika la kimataifa la uhamiaji IOM na serikali ya Chad imebaini kuwa kwenye mpaka baina ya Chad na Nigeria kuna kundi kubwa la watu wa Chad wanaorejea kutoka Nigeria ikiwemo idadi kubwa ya watoto walio peke yao wa kati ya umri wa miaka 6 hadi 14.

Tathimini hiyo imefanyika kwa ombi la serikali ya Chad kufuatia ripoti kwamba maelfu ya raia wa Chad wanakimbia machafuko nchini Nigeria. Tathimini imegundua kwamba idadi kubwa ya wahamiaji kwenye kijiji cha Ngouboua ni watoto waliopelekwa Nigeria na wazazi wao kusomea katika shule za Korani na hawakuwa na mtu yeyetoe isipokuwa waalimu wao wa kidini. Jumbe Omari Jumbe ni afisa wa IOM.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)

 

Shiriki kwenye Dodoso UN News 2021:  Bofya hapa Utatumia dakika 4 tu kukamilisha dodoso hili.

♦ Na iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter