Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mwakilishi wa UM Somalia alaani mauaji ya mkurugenzi wa redio

Mwakilishi wa UM Somalia alaani mauaji ya mkurugenzi wa redio

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa mataifa nchini Somalia Balozi Augustine Mahiga Jumatano amelaani vikali mauaji ya Abukar Mohamed Kadaf, mkurugenzi wa Somaliweyn Radio ambaye amepigwa risasi na kuuawa usiku wa Jumanne katika wilaya ya Wadajir mjini Moghadishu.

Balozi Mahiga ameitaka serikali ya mpito ya Somalia kufanya uchunguzi huru mara moja ili kuwafikisha kwenye mkono wa sheria waliohusika na mauaji hayo.

(RIPOTI YA JASON NYAKUNDI)