Umoja wa Mataifa wazindua mpango wa kupambana na ugonjwa wa Chikungunya

29 Februari 2012

Maafisa wa afya kutoka Umoja wa Mataifa wametoa mwongozo mpya wa kusaidia nchi kwenye mabara ya Amerika kutambua ugonjwa ujulikanao kama chikungunya uanosambazwa na mbu na ambao tayari umewaambukiza zaidi ya watu milioni kote duniani.

Mpango huo uliozinduliwa na shirika la afya duniani WHO ni wa kuwatarisha maafisa wa afya ili kuutambua na kuuzuia ugonjwa huo ikiwa utasambaa hadi kwenye mabara ya Amerika. Hata kama ugonjwa huo haujaripotiwa magharibi mwa dunia, kusafiri kwa abiria kwenda sehemu zilizo na ugonjwa kunaweza kusababisha kusambaa kwake kwenda nchi ambazo haujawai kuripotiwa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter