Maduka ya madawa ya mtandao yatumia mtandao kuwafikia vijana

29 Februari 2012

Bodi ya kimataifa inayohusika na madawa INCB inaonya kuwa maduka haramu yanayotumia mtandao kwa sasa yanawalenga vijana kupitia mawasilino ya mtandao. Hii ilikuwa moja ya ajenda ya ripoti ya mwaka 2011 ya bodi hiyo iliyozinduliwa mjini Vienna.

Rais wa INCB Hamid Ghadse anasema kuwa maduka ya kuuza madawa ya kupitia mtando ukiwemo wa mawasiliano ya Facebook kuwafikia vijana kwa lengo la kuzuia madawa yaliyo haramu. Ripoti hiyo inaeleza kuwa nchi za Caribbean zinaendelea kutumiwa kama vituo vya ulanguzi wa madawa kutoka Amerika kusini hadi nchini Marekani huku maeneo ya kaskazini mwa Afrika yakitumika kupitisha madawa kwenda Ulaya.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter