Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatma ya mazungumzo ya moja kwa moja Palestina-Israel bado iko “gizani”

Hatma ya mazungumzo ya moja kwa moja Palestina-Israel bado iko “gizani”

Umoja wa Mataifa umezitolea mwito Palestina na Israel kuchukua hatua madhubuti kuyatafutia ufumbuzi masuala yanayokwamisha kurejea kwenye meza ya majadiliano na kuongeze kuwa majadiliano yaliyoanzishwa mwezi uliopita yamegota katika wakati hali ya mambo huko Gaza ikisalia kuwa tete.

Kwa mujibu wa mwakilishi wa Katibu Mkuu juu ya masuala ya siasa Lynn Pascoe pande hizo zinapaswa kuchukua maamuzi makini kuzitafutia ufumbuzi changamoto zinazokwaza kurejea upya kwenye majadiliano ya moja kwa moja. Mwanadiplomasia huyo ambaye alikuwa akizungumza mbele ya baraza la usalama, amesema kuwa hatma ya kuwa na mazungumzo ya moja kwa moja iko njia panda.

Mazungumzo ya moja wa moja baina ya pande zote mbili yalikwama mnamo Septemba 2010, kufuatia hatua ya Israel kugoma kusitiza mpango wake wa uendelezaji makazi kwenye maeneo ya Palestina.