Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ni wakati wa Afrika kujitengenezea dawa za HIV na ukimwi: Sidibe

Ni wakati wa Afrika kujitengenezea dawa za HIV na ukimwi: Sidibe

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na masuala ya ukimwi UNAIDS Michel Sidibe amesema umefika wakati kwa Afrika kuanza kutengeneza dawa za kupunguza makali ya ukimwi.

Sidibe amesema kwa kuzalisha dawa hizo Afrika nchi kama Ivory Coast na jirani zake watakwepa tatizo la upungufu wa madawa na kufaidika na gharama nafuu ya dawa hizo.

Ameongeza kuwa kuna haja ya haraka ya Afrika kuwa na shirika moja la madawa litakalohakikisha kwamba kuna uzalishaji wa viwango vinavyostahili vya dawa za HIV kwa ajili ya watu wa Afrika.

Kauli yake imekuja wakati wa mkutano na Rais wa Ivory Coast Alassane Ouattara ambapo bwana Sidibe amekuwa na hofu baada ya kubaini kwamba taifa hilo linategemea sana msaada kutoka nje ili kufadhili vita vya kitaifa dhidi ya ukimwi, hali ambayo inajititokeza katika mataifa mengi ya Afrika.

 Takribani asilimi 87 ya uwekezaji katika masuala ya ukimwi nchini Ivory Coast unafadhiliwa kupitia msaada kutoka nje.