Uchimbaji wa makaa watishia haki za binadamu nchini Bangladesh:UM

28 Februari 2012

Wataalamu huru wa Umoja wa Mataifa wameitaka serikali ya Bangladesh kuhakikisha kuwa sera zinazohusiana na uchimbaji wa mgodi wa makaa zinalinda haki za binadamu. Wataalamu hao wanasisitiza kuwa uchimbaji huo wa mgodi wa Phulbari haustahili kuendelea kutokana na matatizo ambayo huenda ukasababisha.

Pia wanaonya kuwa ukiwa shughuli hiyo itaruhisiwa huenda ikasababisha kuhamishwa kwa maelfu ya watu na kupelekea kuwepo ukiukaji wa haki za binadamu. Kati ya athari zitakazotokana na uchimbaji wa mgodi huo ni pamoja na kukauka kwa visima na kuharibiwa kwa ardhi yenye rutupa.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud