Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya watu wanaoishi kwenye kambi nchini Haiti yapungua

Idadi ya watu wanaoishi kwenye kambi nchini Haiti yapungua

Idadi ya watu wanaoishi kwenye mahema nchini Haiti kufuatia tetemeko kubwa lililoikumba nchi hiyo mwaka 2010 imepungua hadi chini ya watu 500,000. Hii ni kutokana na matokeo ya idara ya nyumba nchini humo wakati shughuli ya kuwahamisha watu hao inapong’oa nanga.

Mpango huo ujulikanao kama 16/6 unawasaidia watu waliopoteza makazi yao wakati wa tetemeko hilo kurejea kwa sehemu 16 zinazotayarishwa hivi sasa. Kwa muda wa majuma mawili yaliyopita familia 200 zimeondoka kabisa kambini. Mpango huu ulizinduliwa na rais Michel Martelly mwaka uliopita na sasa uko chini ya kamati ya serikali.