Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi zaidi ya 30,000 wa Liberia na Ivory Coast kurejea nyumbani

Wakimbizi zaidi ya 30,000 wa Liberia na Ivory Coast kurejea nyumbani

Zaidi wakimbizi 30,000 kutoka Liberia na Ivory Coast wanatarajiwa kurejeshwa nchini mwao kupitia mpango wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM kwa ushirikiano na shirika la kuwahudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR.

Kuna takriban wakimbizi 79,000 kutoka Ivory Coast walio nchini Liberia na wengine 24 ,000 kutoka Liberia wanaoishi nchini Ivory Coast.

Jumbe Omari Jumbe kutoka IOM anasema kuwa shirika hilo linapanga kukamilisha shughuli hiyo kabla ya tarehe 30 mwezi Juni ambayo ndiyo siku ya mwisho ya wakimbizi kutoka Liberia kuendelea kuishi nchini Ivory Coast.

(SAUTI YA JUMBE OMARI JUMBE)