Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban aitaka Angola kuunga mkono vilivyo Umoja wa Mataifa

Ban aitaka Angola kuunga mkono vilivyo Umoja wa Mataifa

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amekamilisha ziara yake nchini Angola ambapo amelitaja taifa hilo kama kiongozi wa kimataifa siku za usoni.

Kwa sasa Angola ndiye mwenyeki wa nchi za SADC na pia kwa jumuiya ya mataifa yanayozungumza lugha ya kireno. Ban anasema kuwa Angola itayafanya mengi kwenye ulingo wa kimataifa kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa ambapo alilitaka taifa hilo kushirikiana na Umoja wa Mataifa kwenye oparesheni zake.

 Ban ameongeza kuwa Angola ina wanajeshi waliopewa mafunzo ya juu na ina vifaa kama ndege zinazohitajika kuwalinda raia wakati wa dharura.

Amesema kuwa ana matumaini kwamba Angola itajiunga na nchi zingine ambazo wakati mmoja zilipata huduma za Umoja wa Mataifa na ambazo kwa sasa zinatoa mchango mkubwa kwa Umoja wa Mataifa.