Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuna zana 23,000 za nyuklia zinazotishia usalama:Iran

Kuna zana 23,000 za nyuklia zinazotishia usalama:Iran

Taifa la Iran limeuambia mkutano kuhusu silaha za maangamizi mjini Geneva kuwa zana za kinyuklia zinaweza kuongezeka hasa wakati baadhi ya mataifa yanaonekana kuwa huru kuyatisha mataifa mengine yakiwemo mataifa yasiyo na silaha hizo.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Ali Akbar Salehi amesema kuwa kuna njia mbili za kuushughulikia mpango wa nyuklia nchini Iran wakati ya kwanza ikiwa ni ushirikiano na kujadiliana huku ya pili ikiwa ni kukabiliana na mizozo.