Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Syria yajiondoa kwenye mjadala wa baraza la haki za binadamu

Syria yajiondoa kwenye mjadala wa baraza la haki za binadamu

Syria imejiondoa kutoka kwenye kikao cha baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kinachojadili ghasia zinazoendelea nchini humo.

Balozi wa Syria Faysal Khabbaz Hamoudi anasema kuwa ujumbe wake haukitambui kikao hicho na kulishutumu baraza hilo kwa kukiuka sheria zake za uongozi.

Balozi Hamoudi anadai kwamba mjadala huo utachochea makundi ya kigaidi yanayoipinga serikali.

(SAUTI YA BALOZI HAMOUDI)