Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la haki za binadamu lataka ghasia zikome Syria:

Baraza la haki za binadamu lataka ghasia zikome Syria:

Akiongea wakati wa kuanza kwa mjadala wa baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa kuhusu hali nchini Syria mkuu wa haki za binadamu kwenye Umoja wa Mataifa Navi Pillay anasema kuwa hali nchini Syria inazidi kuzorota huku vikosi vya serikali vikiendelea kuwadhulumu maelfu ya waandamanaji na watetesi wa haki za binadamu.

Pillay amerejelea wito wake akisema kuwa hali nchini Syria inastahili kuripotiwa kwenye mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita na kuongeza kuwa uhalifu wa kibinadamu unaendelea nchini humo.

(SAUTI YA NAVI PILLAY)

Naye rais wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa Nassir Abdulaziz Al-Nassaer ameelezea hofu kufuatia hali iliyopo nchini Syria hasa kutokana na matumiz ya silaha nzito dhidi ya raia wa nchi hiyo. Amutaka utawala nchini Syria kusitisha mauaji ya raia.