Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto wengi waishia mitaani mijini:UNICEF

Watoto wengi waishia mitaani mijini:UNICEF

Zaidi ya watoto bilioni moja kote duniani wanalelewa mijini huku wale wanaoelelewa kwenye familia maskini wakiwa hawapati huduma muhimu.

Hii ni kwa mujibu wa ripoti ya mwaka huu kuhusu hali ya watoto duniani ya shirika la kuwahudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF.

UNICEF inasema kwamba mmoja kati ya watu watatu walio mijini wanaishi kwenye sehemu maskini za mabanda huku idadi kubwa ya watoto wakiwa hawapati maji safi , umeme na huduma za afya. Peter Smerdon ni msemaji wa UNICEF.

(SAUTI YA PETER SMERDO)